Miongozo ya Jumuiya ya Fiesta

Fiesta ni sehemu ya ukweli na uwazi ya kutafuta wapenzi. Lengo letu ni kuunda mahali ambapo kila mtu anaweza kuonesha uhalisia wake na kile anachotafuta hasa. Tunataka kila mtu afurahie safari yake ya Fiesta, na kutumia jukwaa letu kwa usalama na ustaarabu. Ili kuhakikisha kwamba kila mmoja anafuata utaratibu huo katika jumuiya yetu, tuna miongozo michache ya kufuata.

Onesha uhalisia

Tafadhali uwe mkweli kuhusu wewe ni nani. Tunatumaini kwamba utakutana na watu nje ya mtandao kupitia Fiesta, hivyo utahitaji kutumia jina lako halisi, picha na taarifa katika wasifu wako. Tunapendekeza utumie njia yetu ya kuthibitisha picha ili kuwajulisha wanajumuiya wengine kwamba wasifu wako ni halali – baada ya kukamilika, unaweza kuchagua kuwaonesha wengine wasifu uliothibitishwa tu ✅

Haturuhusu kushirikiana akaunti. Ingawa tunajua kuwa kila mahusiano ni ya pekee sana, huwezi kushiriki akaunti yako ya Fiesta au kuiunda kuwa kama akaunti ya kikundi cha wenzi au marafiki. Hapa ni mahali pa kuonesha uhalisia na utu wako.

Tumia sehemu zetu! Tunazo nyingi sana ndani ya programu yetu na katika tovuti ili kuhakikisha kwamba mazungumzo yako ni ✨. Tafadhali usinakili na kutuma ujumbe uleule kwa kila mtu unayempenda – tumia wakati kuangalia kila mmoja anatafuta nini kwa kusoma maswali yaliyo kwenye wasifu wao au tumia mojawapo ya “vifunguzi vizuri” tulivyo navyo. Unaweza kutambua kuwa wewe ni pacha unayependa kula piza kitandani siku ya Jumapili asubuhi – tushukuru baadaye.

Tenda kwa wema

Tunajitahidi kuwa wawazi kadiri tuwezavyo, katika kila jambo tunalofanya. Tunakuomba na wewe pia ufanye vivyo hivyo - iwapo hutafanya hivyo au kusema kweli katika maisha halisi, basi tafadhali usifanye hivyo mtandaoni.

Hatuvumilii hata kidogo matamshi yanayochochea chuki. Hayo yanatia ndani habari zote zinazozungumzia aina yoyote ya ukandamizaji; ukiwemo (lakini si hayo tu) rangi, ukabila, ubaguzi wa dini, uwezo wa mtu, jinsia ya mtu, umri, asili ya utaifa, jinsia ambayo mtu huvutiwa nayo, au mwingine wowote ambao umekusudiwa kumshambulia mwanachama hususa wa jumuiya yetu. Ikiwa wasifu au mazungumzo yako yana viashiria vya aina yoyote ya mambo hayo, tutafunga akaunti yako daima. Kwa hiyo tunakuhimiza uwe mkweli kuhusiana na kile unachotaka, tafadhali usitumie lugha ya kibaguzi katika wasifu wako. Wema ni ufunguo 💜

Tunza usalama

Usalama wako ndiyo jambo muhimu sana kwetu. Tafadhali usiweke mahali popote pale mtandaoni katika wasifu wako wa umma; jina lako la mwisho, namba ya simu, anwani ya nyumbani au kazini, taarifa za akaunti yako ya barua pepe au mtandao wa kijamii. Unapomtumia ujumbe mtu mpya, tunapendekeza kwamba endeleeni kuwasiliana kupitia programu au tovuti yetu kwa kuwa hapo pana michakato mizuri ya kulinda usalama wako. Unaweza kusoma zaidi kuhusu dondoo zetu za usalama here.

Miongozo ya picha

Picha zinazokuwakilisha wewe kihalisi hufanyiza wasifu maridadi sana. Tafadhali hakikisha kwamba picha unazopakia zinakidhi vigezo hivi:

  • Hazimwoneshi mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18
  • Hazifichi uso wako
  • Hazipaswi kuwa na alama ya maji, nembo, maandishi ya mlazo au uhariri makini
  • Hazina maudhui ya ponografia au ngono dhahiri
  • Huwaweki watu wengine au mashuhuri ambao si wewe (isipokuwa kama kweli wewe ni Beyoncé)
  • Hazioneshi maudhui yoyote batili, ujeuri au kuchukiza

Tunataka ufurahie zaidi unapotumia Fiesta, na kujihisi huru unapojieleza na kutafuta unachotaka, pasipo kumwathiri vibaya mtu yeyote.

Tunatumia mchanganyiko wa mifumo ya kiotomatiki na timu ya wasimamizi ili kusimamia na kupitia akaunti na jumbe zenye maudhui yanayovunja Miongozo hii na Sheria na Masharti yetu. Ikiwa hutaheshimu miongozo yetu au Dhamana ya Unyoofu, tunaweza kuzuia utumiaji wako wa Fiesta au kuondoa daima akaunti yako ya Fiesta (iwe matendo yako yatatokea ukiwa mtandaoni au la).

Tunajivunia kuwa na jumuia kubwa zaidi na inayokua kwa kasi sana katika ulimwengu wa kutafuta wapenzi, na tunatumaini unafurahia kuwa mshirika wa jumuia hii :)